Raisi wangu mpendwa
Milihoi kashuka duniani
Wakaangamiza watakatifu wa kweli
Sasa kila mtu amegeuka shetani ni nguo ya malaika
Maajabu ya firauni sio?
Vipi tukakosa kama tunavyo vyote
Vipi tukafa njaa kaskazini ilhali kusini kwa ng’aa kibichi
Vipi tukawa maskini katika nchi tajiri
Vipi tukakosa maji katika mafuriko
Vipi wengine wakosa madawa ilhali wengine wachagua magari
Vipi kutasoma hadi kileo na kushindwa kuvuna jasho letu
Vipi Rais?
Langu ni kuwaza kama kweli wa tazama taarifa ya habari
Wachanana siasa tazama maisha ya panzi kama mimi
Itakuwa vipi ulale vyema sisi tukiishi kama majitu
Rais vipi maisha kawa magumu na shilingi kawa ngumu kupata
Wengine wakisinzia juu ya shilingi elfu tano kwa siku huko parliament
Vipi biashara yangu ndogo kashambuliwa kila siku
Ilhali wezi wa mali ya serikali wazama katika utajiri wa nchi nzima
Vipi kamiti kajaa na wezi wa vitu vidogo ilhali
Na wanao amri mauaji ya mamia ya watu katembea vifua mbele
Vipi ukawacha vijana wakae bila kazi… ilhali waskia fununu kuwa wanalipwa kutenda dhambi
Eeei Rais? Vipi ukalala salama usiku?
© Namatsi Lukoye
Wetu brings us together, connecting and unifying us through fabric sculptures, dolls, stories, and poetry, symbolizing power and resilience. Experience art rooted in African femininity, healing, and hope.
Wednesday, March 2, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
The girl the world turned from - Owefu Part 3
The Girl the World Turned From Ayuna (not her real name) is a girl with a golden smile. She shakes my hand and sits next to me smiling she d...
-
A woman like me, is rare But not too rare she is there Her intentions are pure and present as her love Love overflowing , her actions consis...
-
In celebration of Women, I join 7 women to portray different types of stereotypes and women in a Play called:- Edge of Womanhood which will ...
-
Give me a cup of peace and maybe then, I will feel better give me a plate of sanity am sure that then, things will go well because right now...
No comments:
Post a Comment